Translate

Monday, November 20, 2017

Riwaya: SIKU TATU KABLA
Mtunzi: PIANO MAYA
CONTACT:0687913339
WhatsApp:0656292416
Dar es salaam
SEHEMU YA PILI(02)
Akajigonga upande wa kichwani katika jiwe lililokuwa limezama chini ya ardhi, na kuchomoza kiasi upande wa juu ya aridhi, na kupoteza fahamu papo hapo, baada ya sekunde kadhaa kupita, wale watu waliokuwa wameshikilia marungu,mawe pamoja na mapanga wakawa wamefika eneo hilo,, bila kuchelewa yule dada akavuta begi lake kutoka mikononi mwa Kangambula , ,punde si punde wale watu wakataka kumshambulia Kangambula,, ghafla ikasika saauti ya yule dada aliyeibiwa begi ikisema,,"muacheni sio huyu,, hata hafanani na yule kijana aliyeniibia begi langu, aliongea maneno hayo huku akijiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu,, mmoja kati waliokuwemo miongoni mwa kundi hilo akamtazama kwa makini Kangambula akagundua ni kweli sio yeye, akageuza shingo yake na kumtazama yule dada aliyeibiwa begi...kisha akasema,"kwa sababu umeshapata begi lako, hakuna shida, baada ya kauli hiyo watu wakatawanyika kila mmoja akapita njia yake na ukimya ukatawala eneo hilo.
baada ya masaa mengi kupita, Kangambula alionekana bado akiwa kalala pale chini,, punde si punde akashtuka na fahamu zikarejea,, akahisi maumivu makali upande wa kichwani,, akanyanyuka taratibu kwa kujikongoja!akaonekana kushangaa eneo hilo,, akajiuliza hapa ni wapi?
kumbe alivyodondoka chini na kujingonga katika lile jiwe ubongo wake ulitikisika na kumbukumbu zake zikapotea,, kwa sasa hakumbuki jambo hata moja.
upande mwingine ,kule nyumbani kwao Kangambula,, alionekana Mbaliwa,,mama mzazi wa Kangambula akiwa na wasiwasi juu ya mwanae,akajisemea moyoni,,"mbona leo kachelewa kurudi nyumbani! yapataa saa kumi na mbili za jioni sasa,, mwanangu kapatwa na nini?
alijisemea maneno hayo akiwa kaketi nje ya nyumba, ghafla ikasikika sauti ya mumewe akikohoa mfululizo,huku akimuita mkewe! sauti hiyo ilitokea chumbani,
Mbaliwa akapata wasiwasi akanyanyuka na kutimua mbio kuelekea ndani ya nyumba akapitiliza moja kwa moja mpaka chumbani...akashtuka kumuona mumewe anajinyoosha kwa nguvu zake zote,,punde si punde akashusha pumzi na kutulia tuli. Mbaliwa akasogea kitandani huku akimuita mumewe,, aliita mara kadhaa huku akimtikisa,, lakini mumewe hakuitika hata hakuamka. ndipo akagundua mumewe tayari kakata roho,, akaangua kilio kwa sauti kali.
Asubuhi palipokucha taratibu za mazishi zikafanyika lakini mpaka muda huu Kangambula hakuwepo nyumbani, pia hajui kama baba yake amefariki! jambo hilo lilizidi kumchanganya sana Mbaliwa,, lakini hakukata tamaa ya kumsubiri mwanae aje nyumbani wajumuike kumzika baba yake!
masaa yalizidi kusonga hatimae muda wa kuzika ukafika lakini hakuna dalili yoyote ya Kangambula kurudi nyumbani,,ikalazimika watu waende kumtafuta Kangambula aje kumzika baba yake. lakini hawakufanikiwa kumpata ... kadri masaa yalivyozidi kusonga ndivyo, maiti ya baba Kangambula ilizidi kuharibika na kutoa harufu kali.. ikalazimika azikwe muda huohuo,,na mazishi yakafanyika.
baada ya siku kadhaa kupita ,,Mbaliwa alikuwa katika majonzi mazito ya kumpoteza mume wake kipenzi,, mbaya zaidi haijulikani ni wapi alipo mwanae!
siku zilizidi kusonga na miezi ikakatika,,hali ya maisha ya familia ya Mbaliwa ikaanza kubadilika! maisha yakawa magumu kwa upande wake,,wakati mwingine walikosa pesa ya kununulia chakula,siku ya leo,Mbaliwa aliwatazama watoto wake wawili aliobakinao nyumbani,,akajikuta analia kwa sababu bado wadogo hawawezi kujitegemea!
************************************
baada ya miaka kumi kupita,, akaoneka kijana mmoja akiwa amebeba mifuko miwili mikubwa,, akazipiga hatua kuufuata mkokoteni wake na kuweka mifuko hiyo iliyojaa takataka,, kisha akaondoka zake..mtu huyo si mwingine ni Kangambula mwenyewe. kumbe miaka hiyo yote alikuwa mjini akifanya kazi ya ubebaji taka kwa malipo.
siku ya leo alifanya kazi ya kubeba taka mpaka majira ya saa kumi za jioni,,katika pitapita zake akagonga hodi katika geti la nyumba iliyokuwa imejitenga... nyumba hiyo ilionekanakumilikiwa na tajiri kutokana na uzuri wa jengo la nyumba hiyo! Kangambula aligonga geti hilo kwa mara kadhaa lakini hakuna alikuja kufungua geti hilo,, akaamua kuchukua mfuko uliokuwa na takataka kando ya geti hilo,,kisha akajisemea moyoni,,"kesho nitakuja kuchukua pesa yangu ya kubeba takataka hizi..akabeba mfuko huo na kuondoka zake..kabla hajafika mbali, akastaajabu kuona magari yamebeba maaskari katika njia hiyo anayopita yeye, akatoka barabarani na kusimama kando ya barabara...akasimama huku akitazama magari hayo,, akaona yamesimama nje ya lile jumba la kifahari..punde si punde maaskari hao wakavamia na kuingia ndani ya jumba hilo huku maaskari wengine wakiwa wamebaki upande wa nje wameshikilia bunduki zao.
Kangambula akaamua kuondoka zake.. akasukuma mkokoteni wake kwa pupa,,ghafla ule mfuko ukadondoka na takataka zote zikamwagika chini Kangambula akashtuka kuona kisu kikiwa na damu pamoja na bastola,,macho yakamtoka,,wakati anatahamaki ikasikika sauti ikisema,"............
ITAENDELEA......
Ungana nami PIANO MAYA katika sehemu ya 3

Saturday, November 18, 2017

Riwaya: SIKU TATU KABLA
Mtunzi: PIANO MAYA
CONTACT:0687913339
WhatsApp:0656292416
Dar es salaam

                           SEHEMU YA KWANZA(01)



hahhahaa we jamaa unanichekesha sana, baba yako hana hata baiskeli alafu wewe unawaza kumiliki gari, acha fikra potofu na ndoto za mchana kweupe!
ilisikika sauti hiyo ya kijana mmoja aliyekuwa ameongozana na KANGAMBULA,walikuwa marafiki walioshibana,, walisaidiana kwa kila jambo, Kangambula akasema,"nitaendelea kusoma kwa bidii ili niweze kuisaidia familia yangu na kuwasomesha kuwasomesha wadogo zangu..

wakati huo huo upande mwingine, nyumbani kwao kangambula ,,alionekana mwanamke mmoja akiwa anatoa furushi la nguo na kuliweka nje kando ya nyumba,, kisha akazipiga hatua kurudi ndani ya nyumba,, jina lake anaitwa Mbaliwa, ni mama mzazi wa Kangambula. akapitiliza moja kwa moja mpaka chumbani akaketi juu ya kitanda huku akimtazama mumewake kwa macho ya huruma, huku akisema , utapona mume wangu, naimani zile dawa alizokupa daktari zitakusaidia kurudisha afya yako kuwa njema kam awali... mimi pia nakuombea kwa Mungu akuponye upone haraka. mumewe akamtazama kisha akasema,"asante mke wangu, kwani Kangambula bado hajatoka shuleni?
mkewe akatabasamu kisha akasema, unampenda sana mwanao, hii ndio mida yake ya kutoka shule, atakuja muda si mrefu, kabla hajamaliza sentensi, ikasikika sauti ya Kangambula ikimuita mama yake,,
bila kuchelewa Mbaliwa akatoka chumbani akija upande wa sebuleni kumsikiliza mwanae, Kangambula akauliza hali ya baba yake huku uso wake ukionyesha shauku ya kutaka kumuona muda huohuo. Mbaliwa akasema," si njema sana pia alikuwa anakuulizia. Kangambula akazipiga hatua kuingia chumbani kumsalimia baba yake.

   ***************BAADA YA MWEZI MMOJA KUPITA***********

Kangambula akasimamishwa masomo, ni baada ya kushindwa kulipa ada ya muhula uliobaki,, pia mwalimu akasisitiza hatofanya mtihani endapo asipolipia kiasi cha pesa kilichobaki! jambo hilo lilimfanya Kangambula kuwa mnyonge na huzuni ikatawala juu yake, mbaya zaidi, zimebaki siku tatu tu, afanye mtihani wa kuhitimu kidato cha nne.aqkaipokea barua kutoka mikononi mwa mwalimu mkuu,, huku machozi yakimtoka, akajaribu kubembeleza huku akitoa sababu za msingi zilizosababisha ashindwe kulipia kiasi cha pesa iliyobaki kwa ajili ya ada,, lakini mwalimu mkuu hakutaka kusmsikiliza akamfukuza,,"toka ofisini kwangu, Kangambula akatoka akalitazama darasa alilokuwa analitumia kwenye vipindi vya masomo, akashindwa kuvumilia machozi yakamtoka, akalia kwa uchungu wa hali ya juu, rafiki yake kipenzi akamuona Kanagambula akilia, akaamua kumfuata na kumfariiji. lakini haikusaidia faraja hiyo haikuweza kutibu jeraha ndani ya moyo wa Kangambula,, hakujibu kitu,"aliishia kumtazama rafiki yake kisha akaamua kuondoka na kurudi nyumbani.

Kangambula alitembea,lakini alikuwa mbali kifikra, akaamua kupiata njia ya mkato ilimradi awahi kufika nyumbani. kwa mbali akaonekana kijana mmojqa anakimbia kwa kasi ya ajabu huku uso wake ukionyesha wasiwasi maradufu! naye pia alikuwa kavalia suruali yenye rangi kama sale ya shule aliyoivaa Kangambula,, wakati kijana huyo anakimbia akadondosha akatupa begi alilokuwa amelishikilia,, kuku akiendelea kutimua mbio na kutokomea kusikojulikana!
Kangambula akastaajabu sana,, hakujali akaendelea kuzipiga hatua kuelekea nyumbani. akafika karibu na lile eneo ambalo yule kijana alitupa lile begi.
akajisemea moyoni,,"bila shaka huyu ni mwanafunzi katika shule ninayosoma mimi. inamaana kapatwa na ugonjwa wa akili? mbona katupa begi lake? ...Kangambula aliwaza hivyo kwa sababu yule kijana alikuwa kavaa suruali yenye rangi kama aliyovaa yeye! hivyo akaamini ni mwanafunzi... lakini hakujali akaendelea kuzzipiga hatua.. baada ya hatua kadhaa jua lilikuwa kali akaamua kuvua shati la shule na kuliweka ndani ya begi akabaki na t-shirt nyepesi. ghafla wazo likamjia,, akaamua kurudi nyuma kulifuata lile begi alifungue atazame jina la mwanafunzi huyo pamoja na kidato.
alipolikaribia begi hilo akasita kulichukua,, akasimama kwa sekunde kadhaa, huku akilitazama,, akalisogelea na kulichukua akafungua zipu ya begi hilo dogo! akashtuka! macho yakamtoka,, akaangaza macho yake huku na kule huku mikono yake ikitetemeka,, jasho jembamba likaanza kumtoka,,, akaliachia begi hilo kisha akachuchumaa,,, uso wake ukaonyesha kuwa na wasiwasi kupita kiasi. pia bado macho yake yaliendelea kutazama huku na kule! hakuona mtu yeyeote kuwepo eneo hilo. akanyanyuka na kuliacha begi hilo. akatimua mbio kukifuata kichaka kilichokuwa kando akatoa begi lake lenye madaftari na kulificha ndani ya kichaka hicho.. kisha akarudi pale lilipokuwepo lile begi lililotupwa na yule kijana!
akialifungua kwa maranyingine tena.. akameza mafundo kadhaa ya mate. kisha akajisemea moyoni,,"hizi ni pesa kweli au naota ndoto za mchanamchana kweupe?
akazishika pesa hizo ,,akagundua ni pesa kweli..noti za shilingi elfu kumi kumi..akalifunga begi hilo akalichukua na kuliweka mgongoni! akajisemea moyon,," sasahivi naenda kulipa ada yote iliyobaki.. alafu naenda nyumbani kumchukua baba yanguu nimpeleke mjini akatibiwe.. baada ya kuwaza hivyo,, akatabasamu kisha akatimiua mbio kurudi shuleni.. kulipa kiasi chote cha ada iliyobaki.

baada ya nusu saa kupi akaonekana akizipiga hatua za haraka haraka kuelekea katika ile njia alipolificha begi lake la shule. akiwa njiani akastaajabu kuona kundi la watu wakiwa wameshikilia marungu na mapanga miongoni mwa watu hao alionekana mwanamke akili kwa uchungu wa hali yajuu,, Kangambula akajisemea oyoni,,"bila shaka huyo mwanamke katenda kosa hivyo wanamuadhibu,, ghafla ikasikika sauti ya yule mwanamke ikisema kwa msisitizo mwizi mwenyewe yule pale na begi langu analo.. sauti hiyo ilimstua Kangambula baada ya kusikia kali ya mwanamke huyo ikihusisha begi..wakati anatahamaki ghafla akaona lile kundi la watu likija upande wake huku wakipiga kelele MWIZIII MWIZII MWIZII! kangambula akaamua kutimua mbio ghafla akajikwaa na kudondoka chini.

ITAENDELEA............


Ungana nami PIANO MAYA(MAYA wa HADITHI) katika sehemu ya 2

Monday, October 16, 2017

New audio song VUMILI-YOZZ PIANO Producerd by Q THE DON